1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHaiti

Baraza tawala la mpito la Haiti kuwa na urais wa kupokezana

Tatu Karema
11 Mei 2024

Baraza tawala la mpito la Haiti linaloongoza taifa hilo lililokumbwa na ghasia, litabadilisha uongozi wake kila baada ya miezi mitano. Hii ni kulingana na nakala ya amri rasmi iliyoonekana na AFP

https://p.dw.com/p/4fjv8
Wanachama wa baraza tawala la mpito la Haiti wakutana kwa mkutano katika ofisi ya waziri mkuu mjini Port-au-Prince, Haiti, mnamo Aprili 30, 2024
Wanachama wa baraza tawala la mpito la HaitiPicha: Johnson Sabin/EPA

Amri hiyo rasmi, imesema kuwa ili kuepusha kasoro zozote katika baraza hilo tawala, wajumbe 9 wamekubaliani kwa kauli moja kuongoza kwa kupokezana.

Maamuzi muhimu yanapaswa kuungwa mkono na wajumbe 5

Baraza hilo pia lilikubali kuwa maamuzi yake muhimu zaidi, ikiwa ni pamoja na uteuzi wa waziri mkuu na serikali, yatafanywa kwa wingi wa kura tano kati ya saba, ambayo ni idadi ya wajumbe wenye haki ya kupiga kura.

Soma pia:Ariel Henry ajiuzulu ili kulipisha baraza la mpito kuanza kazi

Kiongozi wa sasa wa baraza hilo Edgard Leblanc ataliongoza baraza hilo hadi Oktoba 7, na kufuatiwa na wanachama Smith Augustin, Leslie Voltaire na Louis Gerald Gilles katika usanjari huo.

Amri hiyo rasmi, imeongeza kuwa uwiano ndani ya barazahilo la mpito ni hitaji kuu la kuhakikisha suluhisho kwa mzozo wa pande nyingi unaolikabili taifa la Haiti.