1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Janga la ugonjwa wa kifaduro lafagia Ulaya

8 Mei 2024

Mataifa ya Ulaya yameripoti ongezeko la ugonjwa wa kifaduro mwaka 2023 na robo ya kwanza ya mwaka huu 2024, wakati maambukizi ya ugonjwa huo yakiwa mara 10 zaidi tofauti na ilivyokuwa miaka miwili iliyopita.

https://p.dw.com/p/4fdEr
ECDC
Wagonjwa 60,000 wa kifaduro wameripotiwa barani Ulaya katika mwaka wa 2023Picha: Jonathan Nackstrand/AFP

Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa barani Ulaya kimesema kuwa, wagonjwa 60,000 wa kifaduro wameripotiwa barani Ulaya ndani ya muda wa mwaka jana hadi robo ya kwanza ya mwaka huu huku watu 19 wakifariki dunia, wakiwemo watoto wachanga 11 na watu wazima wanane.

Soma pia: Watoto milioni 20 hawapati chanjo ya magonjwa hatari

Nchini Uingereza, kwa mfano, wataalamu wa afya wametahadharisha kuwa visa vya ugonjwa huo unaothiri zaidi mapafu huenda vikaongezeka na kufikia kiwango cha juu zaidi katika muda wa miaka 40.

Ugonjwa wa kifaduro ni maambukizo ya bakteria yanayoathiri mapafu na mfumo wa kupumua na huathiri watu wa rika zote ingawa watoto wachanga na wazee ndio walioko kwenye hatari zaidi.