1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Xi wa China yuko Serbia kuimarisha ushirikiano

8 Mei 2024

Rais Xi Jinping wa China anatarajiwa kufanya mazungumzo na mwenzake wa Serbia, Aleksandar Vucic, mjini Belgrade leo wakati Beijing inanuia kuimarisha uhusiano wake na mataifa ya Ulaya.

https://p.dw.com/p/4fcFA
China na Serbia ni washirika wa karibu
China imemwaga mabilioni ya fedha nchini Serbia na nchi jirani za Balkan, hasa katika sekta za madini na viwandaPicha: Darko Vojinovic/AP Photo/picture alliance

Kiongozi huyo aliwasili katika mji mkuu wa Serbia Jumanne usiku baada ya kufanya ziara nchini Ufaransa iliyoshuhudia mazungumzo kati yake na Rais Emmanuel Macron kuhusu biashara na uhusiano wa karibu wa China na Urusi katikati ya vita nchini Ukraine.

Soma pia: Rais Xi wa China akosoa NATO kabla ya ziara yake ya Serbia

China imemwaga mabilioni ya fedha nchini Serbia na nchi jirani za Balkan, hasa katika sekta za madini na viwanda na mwaka uliopita, Beijing na Belgrade zilitia saini makubaliano ya biashara huria.

Waziri wa fedha wa Serbia, Sinisa Mali, ameliambia shirika la utangazaji la RTS kuwa mazungumzo kati ya Rais Xi na Aleksandar Vucic yatajikita katika kile kilichoitwa "mradi mkubwa."